Habari z'asubuhi 15 Aprili, 2025
- Kinshasa: Rais wa Jamuhuri anakataza mawaziri kusimamisha kazi viongozi wa makampuni ya serikali kabla hajapewa taarifa kuhusu maamuzi hayo
- Bunia: Huko Ituri, zaidi ya walimu na viongozi mia nne wa shule ya msingi walishiriki katika awamu ya kwanza ya mtihani wa kimashindano ya kitengo kidogo cha elimu ya kitaifa na uraia mpya katika mji wa Bunia siku ya sita
- Goma: Jimboni Kivu Kaskazini - Karibu watu watatu waliuawa katika familia moja na watu wenye silaha usiku wa kuamkia hii siku ya kwanza tarehe kumi na ine Aprili katika katika Kata Majengo, mjini Goma.