Hali ya kukatisha tamaa ya vilima vya taka taka vilivyotawanywa hovyo mjini Beni, inatia wasiwasi viongozi wa mitaa wa Kata Nzuma. Kwa Josué Kapisa, mkuu wa kitongoji hiki, hatari za kiafya ni kubwa kwa wakazi wanaozunguka kwa sababu hakuna hatua za kuzuia zinazochukuliwa na viongozi ili kusimamia ipasavyo taka taka hizo katika eneo lake. Josué Kapisa, mkuu wa Kata Nzuma katika manispa Ruwenzori katika mji wa Beni, ndiye mgeni wetu wa siku, anazungumza na Marc Maro Fimbo.
/sites/default/files/2024-09/011024-p-s-invitebenijosuekapisaqnzuma-00-web.mp3