Justin GUDZA: Kuwa na ukabila haitasaidiya

 

 

Huko Ituri, kiongozi wa sekta ya Walendu Djatsi ameanzisha mikutano tangu takriban mwezi mmoja sasa na wenzake kutoka jamii zingine za eneo hilo katika tarafa la Djugu. Kusudi: ni kuvunja kutoaminiana kati ya watu wa makabila tofauti na kuimarisha mshikamano wa kijamii katika eneo hilo. Hii ni licha ya kuzuka upya kwa ukatili wa makundi yenye silaha uliorekodiwa katika muda wa wiki mbili zilizopita. Je, ni matokeo gani ya mbinu hii, changamoto na masuluhisho ya amani ya kudumu katika tarafa la Djugu? Justin GUDZA, kiongozi wa Walendu Djatsi anazungumza na Isaac REMO.

/sites/default/files/2025-03/030325-p-s-invitebuniajustingudzawalentudjatsi-00-web.mp3