Habari za siku ya kwanza asubuhi tarehe 19/12/2022
- Uchokozi wa Rwanda kuelekea DRC kupitia M23 unaalikwa kwenye COP15. Mkusanyiko wa kumi na tano ya wanaohusika na utaratibu wa Biodiversite wa umoja wa kimataifa utafanyika pa Montreal, inchini Canada.
- Jimboni Kivu ya kaskazini : kamisheni ya haki za binadamu, sehemu ya Rutshuru, inasikitishwa na ukiukwadji wa haki za binadamu ndani ya kambi za wAkimbizi tarafani Nyiragongo.
- Katika jimbo la Kivu ya kaskazini, kikundi cha watembeza pikipiki wanashutumu usalama mdogo na unyanyasaji wa kila mara wa maaskari jeshi kuhusu wanamemba wao.
- Mji wa bandundu, mji mkuu wa jimbo ya Kwilu, inaorozesha watu wanane waliokufa kati ya wahami waliohama kwa ajili ya vita kutoka Kwamouth huko Maindombe na Bagata huko Kwilu.
- Mjini Matadi, Mfuko wa umoja wa kimataifa kwa watoto UNICEF, imepatia vifaa vya kuwarudisha ndani ya jamii watoto mia moja makumi tatu na tano ambao hawasomi tena.
- Operesheni za kutambulisha na kuorozesha wachaguzi inaanza juma hii, siku ya sita tarehe 24 desemba mwaka tunao.
- Huko kasai oriental, wikendi iliyopita kulizinduliwa kukamata picha Schoolap. Ni teknolojia mpya kuhusu kuandikishwa kwa wanafunzi watakao fanya mtihani wa taifa EXETAT 2022-2023. /sites/default/files/2022-12/19122022-p-s-journalswahilimatin-00_web_.mp3