Habari za jioni 31 Machi, 2025
- Kinshasa: Mfuko wa Kitaifa wa Fidia kwa Wahasiriwa wa Unyanyasaji wa Kijinsia Unaohusiana na Migogoro (FONAREV) unaanzisha Mazungumzo juu ya utambuzi wa mauaji ya kimbari ya Kongo hii siku ya kwanza tarehe makumi tatu na moja Machi mjini Kinshasa
- Bunia: Wanajeshi wa Uganda walitumwa kwa mara ya kwanza Jumapili huko Bule, mji mkuu wa Sekta ya Bahema Badjere jimboni Ituri, ambayo inahifadhi zaidi ya watu elfu Mia moja waliokimbia makazi yao. Walikaribishwa kwa shangwe na wakazi
- Bandundu: Kampeni za uchaguzi wa maliwali, makamu wa maliwali na maseneta wa jimbo la Kwilu, iliyoanza tarehe makumi mbili na tisa Machi, zinaendelea kama kawaida hadi sasa. Uchaguzi huo unakuja baaya ya kurudishwa nyuma kutokana na vurugu za Yakoma na Kwilu./sites/default/files/2025-03/310325-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3