Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 19/12/2022
- Katika jimbo la Ituri, karibu maiti makumi mbili bado zimelala chini katika baadhi ya vijiji vya usultani wa Walese Vonkutu katika tarafa la Irumu.
- Katika jimbo jirani la Kivu Kaskazini, Mapigano yalianza tena siku ya kwanza hii kati ya M23 na wanamgambo wa eneo wa kundi la Nyatura CMC katika kijiji cha Mudugudu, karibu na Mulimbi katika tabaka Tongo, jirani ya Bishusha.
- Katika tarafa la Rutshuru jimboni Kivu kaskazini, usultani wa Bwito, kiongozi mwakilishi wa gavana huko Bambo analaani unyanyasaji, hasa uporaji wa mali katika vijiji vinavyokaliwa na M23.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini ambako tunasalia, watu wakimbizi wa vita wanaoishi katika maeneo tofauti katika tarafa la Nyiragongo wanamuarifu gavana wa kijeshi wa mkoa kuhusu visa vya ukosefu wa usalama ambavyo vimekuwa vikitokea mara kwa mara ndani na karibu na maeneo hayo.
- Kuna hali binadamu wanapitia lakini hazijafanywa ili zidumu. Hii ni sauti ya familia za wakimbizi kutoka Rutshuru, ambazo kwa sasa zinaishi katika kanisa la Kiprotestanti huko Kanyaruchinya, karibu na Goma.
- Na kisha tunasikia kwamba jumuiya za kiraia na viongozi wa utawala wa kisiasa wa majimbo ya Haut na Bas-Uélé wanatoa wito kwa serikali ya Kongo na jumuiya ya kimataifa kuunga mkono wahanga na walionusurika mauaji ya LRA.
- Katika Jimbo la Kivu Kaskazini, tatizo la malisho mabaya linabaki kuwa sababu kuu ya visa vingi vya magonjwa vinavyosababisha vifo ambavyo gereza la Kakwangura katika jiji la Butembo limekuwa likirekodi tangu siku chache sasa. Uthibitisho huo ulitolewa siku ya tano iliyopita kwa Redio Okapi na daktari mkuu wa mtaa wa afya wa Butembo.
- Sherehe za mwisho wa mwaka tayari zimetangazwa mjini Kinshasa katika maduka makubwa mengi. Wengi wameweka mti mkubwa wa Krismasi uliopambwa kwenye mlango./sites/default/files/2022-12/191222-p-s-journalswahilisoir-00_web_.mp3