Habari z'asubuhi 8 Aprili, 2025
- Kinshasa : Rais wa Jamuhuri Felix Tshisekedi aliwatembelea wahasiriwa wa mafuriko mahali wanahifadhiwa mjini Kinshasa jana siku ya kwanza. Alisindikizwa na mke wake
- Kinshasa : Ufunguzi wa kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Mahakama la Kongo ulifanyika hii siku ya kwanza. Sherehe iliongozwa na rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
- Bunia : Huko Ituri, watu wengi wanakufa katika kambi ya wakimbizi ya Kigonze mjini Bunia tangu mwanzoni mwa mwaka huu kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya. Redio Okapi ilitembelea kambi hiyo hii siku ya kwanza tarehe saba aprili, siku ya kusherekea afya duniani.