" Kura ya uwingi kwa kipindi kimoja na kwa mzunguko wa pili ni nini ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” Kura ya uwingi kwa kipindi kimoja na kwa mzunguko wa pili ni nini ? ”

* Kufatana na mafasirio tunayo,kura ni uchaguzi kwa njia ya alama ao ya vyeti vyenyi kutumbukuzwa ndani ya kibweta ao sanduku,ambamo tena vinaondoshwamo na kuhesabiwa.Tukirudilia ulizo lako,husimulia juu ya kura ya uwingi kwa mzunguko wa kwanza, wakati viti vya madaraka vilivyopangwa vinachukuliwa na wakandidenti waliopata ushindi unao lingana na sauti.Kwa kuelewa vizuri inafaa kujua kwa mfano, ikiwa kama kila eneo la uchaguzi,likiwa hivi tawi la msingi kwa uchaguzi,likichagua kandidenti mmoja. Kwa upande ungine,husimulia juu ya kura ya uwingi kwa mzunguko wa pili ao kipindi cha pili, wakati wakandidenti wanachaguliwa kwa kura ya mzunguko wa kwanza na ikiwa walijipatia nusu ya sauti kujumulisha na moja kulingana na sauti zilizojulishwa. Ikiwa kama hakuna hata kandidenti mmoja aliyeweza kupata sauti zile, kura ya mzunguko wa pili huenda kufanyika. Watashiriki kwa kipindi hiki cha pili ni wakandidenti waliopata sauti nyingi wakati wa kura ya mzunguko wa kwanza.Kulingana na hatua hiyo,atatangazwa kama anachaguliwa kwa kura ya sehemu ya pili mkandidenti aliyepata sauti nyingi kufatana na idadi ya sauti zilizojulishwa.

” Basi ndugu, Dunia Mukunda Milemba, mafaa gani na vinyume gani kura ya uwingi kwa kipindi cha kwanza inayo ? ”

* Karynne Kakasi,inafaa kuelewa kama mafaa ya kura kwa uwingi wakati wa kipindi cha kwanza ao mzunguko wa kwanza,mafaa yake basi ni hii,inasaidia upesi kwa kuunda serkali ya watu wenyi kutoka katika makundi mengi, serkali ya nguvu na yenyi kustarehe. Vinyume vya kura hiyo ni kutambua kama makundi madogo ya siasa hayapate ginsi ya kupewa viti vya madaraka.

” Bwana Dunia Mukunda Milemba, tungetamani utuelezee ni kazi gani raisi mpya mwenyi atachaguliwa atafanya mbele ya kuchukua madaraka yake kiserkali ? “.

* Karynne Kakasi,sheria kuhusu uchaguzi inahakikisha kama mbele ya kuchukua kiserkali madaraka yake, raisi mpya wa jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo, anahapa kiapo mbele ya korti kuu ya sheria akisema hivi-mimi,bwana ao bibi fulani, niliye chaguliwa kuwa raisi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo, nahapa kiserkali mbele ya Mungu na rahiyarn-kuchungua na kukinga katiba na sheria ya jamuhurirn-kwa kulinda uhuru wake na eneo lote lakern-kwa kuchunga umoja wa taifarn-kwa kujiachiliya ili niongozwe na moyo wa manufaa kuu na heshima ya haki ya mtu mwanadamu rn-kwa kutumia nguvu zangu zote kwa ukingo wa haki ya rahiya na ya amanirn-kwa kutimiza katika uhaki na hekima kama mtumishi wa rahiya,kazi kubwa ninazopewa.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes courtesrnTél : 00243998909787rnE-mail : [email protected] [email protected]