Tunamkaribisha mgeni wetu Daktari Kahatwa Neema, daktari wa magonjwa ya akili kutoka kituo cha magonjwa ya mishipa ya fahamu cha Goma kinachojulikana kwa jina la kituo cha afya ya akili TULIZO LETU. Wakati ambapo wakazi wa Kivu Kaskazini wanakabiliwa na matukio ya vita, kituo hiki kinaamini kwamba msaada wa kisaikolojia, hasa kwa wakazi wa Goma na kando kando, ni muhimu. Hivyo basi; Kituo hiki kinawaita wakazi wa Goma kuanzia mwanzoni mwa wiki hii kwa ajili ya mashauriano haya ya bure ambayo ilizinduliwa tarehe makumi mbili na ine Machi. Mgeni wetu Daktari Kahatwa Neema anatueleza mengi. Ni katika mahojiano haya na Bernardin Nyangi.