
Radio Okapi/Ph. Marc Maro Fimbo(Photo d'illustration)
Vijana wengi, wakiwemo watoto wadogo, wanajihusisha na ngono pa Jina, eneo lilio kwa umbali wa kilomita makumi ine na tano kutoka Bunia, jimboni Ituri. Hii ni kutokana na kuwepo kwa soko la usiku ambalo linafanya kazi kila siku katika eneo hilo na kuvutia watu. Zoezi ambalo linashika kasi, kulingana na shuhuda za wakaazi. Je, tunawezaje kupambana na tabia hii inayokwenda kinyume na haki za watoto? Hili ndilo swali ambalo Redio Okapi ilimuuliza mkuu wa mashirika ya kiraia wa pahali. Yered Maki anazungumza kuhusu hili na Jean Claude LOKY DILE.