Mchungaji Jems BIENSI : Ndugu zetu wanaoendelea kubeba silaha na kuleta maafa waachane na ile maneno

"Serikali haijawahi kushughulikia kikamilifu tatizo la migogoro ya jamii inayoendelea katika jimbo la Ituri, ambayo ndiyo chanzo cha mauaji ya raia wasio na hatia na uchomaji wa nyumba, hasa katika tarafa la Djugu." Huu ndio ujumbe mkuu kutoka kwa mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Re-Bâtisseur, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Bunia. Mgeni wetu, Mchungaji Jems BIENSI, anaonyesha kwamba wakati umefika wa kulikabidhi tatizo la Ituri kwa muumba: kumwomba neema yake, kwa ajili ya upatanisho wa wana na binti wa jimbo hili na Wakongo kwa ujumla. Anatoa wito kwa viongozi wa makundi yenye silaha kuacha kuwaua ndugu zao wenyewe. Anazungumza na Ezechiel MUZALIA.

/sites/default/files/2025-02/200225-p-s-invitebuniapasteurjemsbiensi-00-web.mp3