Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini: wakati familia nyingi za wakimbizi zikirejea katika vijiji vyao karibu na Kanyabayonga kufuatia mapatano ya kibinadamu, shirika la kupiganisha vifaa via kulipuka (Sylam) linapiga yowe kwa kusema kwamba Maeneo haya ya kurudi, ambayo zamani yalikuwa maeneo ya mapigano, huenda yakawa na vilipuzi . Watoto wawili walifariki siku ya pili iliyopita baada ya kukanyaga kifaa kiakulipuka katika eneo hilo. Kufuatana na hatari hii, Sylam anaomba watu hawa waorejea kuwa waangalifu kabisa. Trésor Hakizimana, kiongozi wa mradi wa “Elimu” katika shirika hilo la Sylam, anaelezea hatua za kufuata ili kuepuka ajali zinazohusishwa na vilipuzi . Anazungumza na Rosalie Zawadi./sites/default/files/2024-07/tresor_hakizimana_web.mp3