Katika jimbo la Kivu ya Kusini, shirika DYNACOD-RDC linachukua hatua za kisheria dhidi ya watu wasiojulikana kuhusiana na ongezeko la moto katika mji Bukavu. Shirika hilo linatambua takriban kesi makumi mbili ya moto iliyojitokeza katika mji wa Bukavu, na kuharibu karibu nyumba elfu moja zilizochomwa moto kwa chini ya miezi kumi. Patient Bashombe, mratibu wa Shirika la DYNACOD-DRC anaomba wakuu wa mahakama kufanya uchunguzi makini wenye lengo la kuwakamata wahusika wa vitendo hivyo ili waaazibiwe . Mwalikwa wetu Patient Bashombe anazungumza na Jean Kasami./sites/default/files/2024-07/patientbashombe_web.mp3