Huko Beni, jumuiya ya kiraia ya mji na wilaya ya Beni ilizindua siku chache zilizopita shughuli ya kizalendo ya kuwaunga mkono wanajeshi wa FARDC na Wazalendo wanaopambana na waasi upande wa Kaskazini mwa jimbo la Kivu Kaskazini. Mpango huu unajumuisha kukusanya chakula na vitu visivyo vyakula, lakini pia madawa. Shughuli hii inakuaje? Tunazungumza juu yake na Brigitte Batapowa, anayehusika na uhamasishaji ndani ya uratibu wa miji wa asasi za kiraia, katika mahojiano haya na Marc Maro Fimbo.
/sites/default/files/2025-02/210225-p-s-invitebenibrigittebatapowa-00-web.mp3