Jocelyne: Kazi ambayo nimejifunza gerezani itanisaidia kimaisha siku nitatoka.

Kitengo cha usaidizi cha utawala wa magereza cha MONUSCO kimeanzisha mafunzo mengi ya kufanya kazi ndani ya gereza la wanawake la Beni. Katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Wanawake Duniani tarehe nane Machi, wafungwa wa kike walionufaika na mafunzo haya walionyesha vitu walivyotengeneza baada ya mafunzo. Mmoja wao, ambaye tutamwita Jocelyne, anaelezea manufaa ya kujifunza huku kama sehemu ya kuunganishwa kwake katika jamii. Tunamsikiliza katika mahojiano haya na Sadiki Abubakar.

/sites/default/files/2024-03/130324-p-s-invitebenifemmedetenue8mars-00-web.mp3