Celestin Sawasawa, kiongozi wa shirika ya raia ya Kilya mtaani Beni

Katika eneo la Beni, hali ya usalama imeimarika sana siku hizi katika eneo la Kilya, ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita. Ni Célestin Sawasawa, kiongozi wa kiraia ya eneo hilo, ambaye anasema hivi. Anaongeza kuwa mbali na visa vichache vya unyanyasaji  hufanywa na waasi ADF, uharakati wao umepunguka sana katika eneo hilo. Wakati wa mkutano kuhusu  usalama wa MONUSCO siku ya pili katika eneo hili, kwa kutarajia kufungwa kwa kambi yake ya kijeshi, jumuiya ya kiraia ya Kilya iliomba urithi mzuri kutoka kwa serikali. Célestin Sawasawa anazungumza na Sadiki Abubakar./sites/default/files/2024-01/invite_swahili_celestin_sawasawa_web.mp3