Astride Kavira, muuguzi mjini Goma.

Astride Kavira, ni mama mwenye umri wa miaka makumi tano na ni muuguzi  huko Goma. Anaendelea vyema sasa, lakini imembidi kupambana na cancer kishujaa kwa takriban miaka mitano sasa. Anaamini kuwa cancer ya matiti "siyo mauti" na "inaweza kupona". Astride Kavira ndiye mgeni wetu, katika kuadhimisha siku maalumu ya mapambano ya kimataifa dhidi ya ugonjwa huu, iliyo sherekewa tarehe kumi na tisa Oktoba mwaka huu. Anakumbuka pigano lake lisilo na kikomo la kushinda cancer ya matiti, kwa msaada wa madaktari wake wanaomtibu. Tumsikilize katika mahojiano haya na Jules NGALA./sites/default/files/2022-10/21102022-p-s-inviteeastridekavirasurvivantecancerdesein-00_web.mp3