Journal matin

Habari za siku ya inne tarehe 11/ 07/2024

  • Katika jimbo la Tshopo, wakazi wa Opienge na Balobe katika mtaa wa  Bafwasende  zaidi ya kilomita mia mbili na makumi sita  mashariki mwa Kisangani, wanaanza kurejea hatua kwa hatua katika maeneo yao.
  • Katika jimbo la Ituri, karibu familia elfu mbili za wakimbizi  ambazo zimepoteza kabisa matumaini ya kurejea katika vijiji vyao vya asili katika eneo la Djugu, wameamua kuhamishwa katika maeneo yao ya makimbilio.
  • Baraza la Maungamo ya Kidini la Ituri, CCRI, lanatoa wito kwa wakaaji  kuongeza umakini ili kuimarisha usalama jimboni  Ituri.
  • Katika jimbo ya Kivu la Kaskazini, visa vya ulipizaji kisasi maarufu hurekodiwa karibu kila wiki katika mji wa Goma na mazingira yake tangu miezi kadhaa.
  • Kilalo kipya kiliwekwa siku ya pili  kwenye Mto Lubi huko Kena Kuna, mji mkuu wa eneo la Kabeya Kamuanga katika jimbo la Kasai Oriental.
  • Kwa zaidi ya wiki moja , maji ya Regideso haitoke katika mji wa Kananga jimboni Kasai-central.
  • Jimboni Koongo central , Kushuka kwa maji ya Mto Kongo inasababisha ukosefu wa maji ya kunywa katika mji wa Matadi.
  • Mahakama ya Katiba imekuwa ikipokeya  tangu  siku ya pili tarehe kenda mwezi huu wa saba wanamemba  wa serikali ambaye wanakuja kuonesha mali zao.
  • Shirika linaoitwa Casmia Casmia  linaohusika na ma maswala la Uchimbaji Madini, linalaani uchimbaji haramu wa madini unaofanyika Kakanda katika jimbo la Lualaba./sites/default/files/2024-07/110724-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3