Habari za siku ya pili asubuhi tarehe 04/04/2023
- Huko jimboni Kivu ya Kusini ambako kisa kingine cha ajali kilihesabiwa kwenye Ziwa Kivu na kusababisha vifo na watu kupotea. Tukio hilo limetokea usiku wa tarehe mbili hadi tarehe tatu mwezi wa inne mwaka huu tunao katika mtaa wa Idjwi.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, karibu watu makumi mbili walikufa katika maporomoko ya udongo jana siku ya mungu huko Bulwa, katika eneo la Buabo mtaani Masisi.
- Katika jimbo la Sankuru, wanawake sita walikufa na wengine inne kujeruhiwa vibaya, hii ni matokeo ya maporomoko ya udongo yaliyotokea Jumapili katika eneo la Telecom katika mtaani Kabondo huko Lusambo.
- Kuliandaliwa Siku bila teksi za pikipiki siku ya kwanza hii katika mji wa Muanda jimboni Kongo Central .
- Katika jimbo la Tshopo, kazi za majengo kuhusu mradi wa maendeleo wa mitaa mia moja na makumi ine na tano zilizinduliwa mwishoni mwa wiki hii huko Isangi, mji mkuu wa mtaa wa Isangi inaopatikana kwenyi kilomita mia moja makumi mbili na tano na mji wa Kisangani .
- Katika Jimbo la Tanganyika, mgogoro wa mpaka unapinga eneo la Kalemie na lile la Nyunzu.Sababu ya mzozo huu ni , ugunduzi wiki chache zilizopita wa amana ya Coltan katika kijiji cha Sango Mutosha kilichoko kwenye mpaka kati ya maeneo hayo mawili.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, vikosi vya Wanajeshi wa Sudan ya Kusini viliwasili Goma siku ya mungu na siku ya kwanza hii , ili kuimarisha nguvu ya jeshi la EAC.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, kujiondoa kwa waasi wa M23, tangu siku ya mungu , kunathibitishwa na duru kadhaa za eneo la Bambu. Hali hiyo hiyo huko Kishishe, katika usuklutani wa Bwito, ambapo raia mia moja waliuawa mnamo mwezi wa kumi na moja mwaka uliyopita.
- Liwali makamu wa Jimbo la Ituri, Alongaboni Benjamin, sasa ndiye mkuu mpya wa polisi wa kitaifa inchini Kongo ya Kidemokrasia ./sites/default/files/2023-04/04042023-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3