Journal Soir

Habari za siku pili jioni tarehe 20/12/2022

  • Jimboni Kivu ya Kusini, hali ya kijamii na kiuchumi inazidi kuwa ngumu katika tarafa la Kalehe, wakati sherehe za mwisho wa mwaka tunao zinakaribia.
  • Katika jimbo la Kasai Oriental, bei ya vyakula vingi  pamoja na bidhaa za viwandani imepanda kwenye soko la Mbuji-Mayi.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, utulivu ilionekana hii siku ya pili asubuhi katika eneo la Mulimbi na Rusekera katika tabaka Tongo, usultani wa Bwito.
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, viongozi wa eneo wa usultani wa Bukumu katika tarafa la Nyiragongo wanapeana hekta makumi tatu kwa jumuiya ya kibinadamu.
  • Watu  wanane wanaodaiwa kuwa ni wezi walichomwa moto wakiwa hai katika muda wa wiki mbili katika mji wa Kalemie.
  • Katika jimbo la Kivu ya  Kusini… Hakuna kazi ilifanyika hii siku ya pili katika jiji la Uvira na katika tarafa.
  • Chama cha kisiasa cha Ensemble pour la République kinaandaa kongamano lake siku ya pili mjini Lubumbashi.
  • Kuhusu uandikishaji wa wapiga kura katika jimbo la Kwilu. Zaidi ya vituo elfu moja mia ine vya kujiandikisha vimepangwa kwa ajili ya utambuzi na uandikishaji wa wapigakura utakaoanza tarehe makumi mbili na ine  Desemba.
  • Katibu Mtendaji wa Mkoa wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Kongo central, alisema yuko tayari kwa shughuli ya utambuzi na uandikishaji wa wapigakura, kwa mujibu wa kalenda ya uchaguzi iliyotangazwa hivi karibuni na kiongozi wa kitaifa wa taasisi hii ya kusaidia demokrasia./sites/default/files/2022-12/20122022-p-s-journalswahilisoir-00_web_.mp3