Journal Soir

Habari za siku ya kwanza jioni 

  • Rais wa Kongo Félix Antoine Tshisekedi amezungumza siku ya kwanza hii asubuhi na mwenzake wa Kenya William Ruto aliye ziarani hapa Kinshasa kuhusu kujitolea kwa mataifa hayo mawili kutafuta amani katika eneo la mashariki mwa DRC.
  • Aliwasili jana Jumapili katika mji mkuu wa Kongo, William Samuel Rutho alizungumza na mkuu wa nchi Felix Antoine Tshisekedi siku ya kwanza hii kunako  cité de l’union africaine kuhusu masuala ya ushirikiano wa nchi mbili na hali ya usalama Mashariki mwa Congo
  • Huko Kivu Kaskazini, hali ilisalia kuwa shwari siku nzima ya siku ya kwanza hii katika eneo la Kibumba. Bunduki zilinyamaza baada ya mapambano ya siku ya Jumapili kati ya FARDC na waasi wa M23.
  • Katika Kivu Kusini, Uratibu wa Mkoa wa P-DDRC-S unalaani na kukashifu vitendo vya kigaidi ambavyo ujumbe wake uliathiriwa siku ya sita iliyopita katika tarafa la Fizi.
  • Chama cha Force de Résistance Patriotique pour l'Intégrité du Congo (FRPI/C) , kinalaani kile inachoita kuwa ni kuridhika na unafiki wa jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na janga la kibinadamu ambalo linatikisa eneo la mashariki mwa DRC kutokana na vita visivyo vya haki vya uchokozi.
  • Kulizinfuliwa  siku ya Jumapili hii huko Matadi katika Kongo centrale, wa mafunzo ya ngazi ya pili kuhusu marekebisho ya faili la uchaguzi, kwa wafanyakazi wa ukatibu wa mkoa wa tume huru ya taifa ya uchaguzi CENI pamoja na wafanyakazi wa shughuli mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.
  • Katika Kwilu, kulizinduliwa jana Jumapili makumi mbili Novemba mwaka tunao katika kituo cha Ntombwa pa Bandundu mjini, kwa mafunzo ya ngazi ya pili  ju ya marekebisho ya faili la uchaguzi, operesheni itakayoanza Desemba ijayo.
  • Katika jimbo la Maniema, shule ya msingi ya CEWIS ya KABOLONGO katika tabaka CHAMBI, usultani wa Bangengele katika tarafa la Kailo imepewa mabati kwa ajili ya ukarabati wa paa lake lililo katika hali mbaya sana./sites/default/files/2022-11/211122-p-s-journalswahilisoir-00_web_.mp3