Habari za siku ya inne jioni
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, sehemu ya mji wa Kibumba inachukuliwa tena, siku ya tano hii na jeshi la Kongo
- Jeshi la Uganda linatayarisha kutuma wanajeshi wengine nchini Kongo kwa niaba ya kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
- Watu sita akiwemo mwanamke mmoja walifariki kwa kupigwa risasi na wengine wanne kujeruhiwa vibaya .
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, msimamizi wa huduma ya itifaki yani protocoli wa gavana wa kijeshi amefungwa siku ya tano hii mjini Kinshasha.
- Serikali la Jimbo la Kwilu ilikabizi rasmi jana siku ya inne vifaa vya shule na bidhaa nyingine kwa watoto wahama , wahanga wa ukatili wa mtaa wa Kwamouth, walioandikishwa katika shule za Bandundu, mji mkuu wa jimbo hili.
- Mjini Beni, suala la vita dhidi ya rushwa lilikuwa lilizungumziwa wakati wa kikao cha kujadiliana leo hii siku ya tano kilichoandaliwa na shirika lliitwao bunge la vijana kwa ushirikiano na offisi ya masuala ya kisiasa ya MONUSCO.
- Bunge la jimbo la Lualaba lilichaguwa wakati wa kikao cha jana siku ya inne azimio linalomuruhusu mwendesha mashtaka wa umma kufungua kesi dhidi ya liwali Richard Muyej na kufunguliwa kwa kesi zidi ya mwanabunge jimboni Louise Mueleshi kwa wizi wa pesa zilizokusudiwa kuunga mkono mradi wa kilimo wa mwaka elfu mbili na kumi na kenda – elfu mbili na makumi mbili .
- Jimboni Ituri, wafungwa watatu wa gereza kuu la Mambasa walifariki jana siku ya tatu katika hospitali kuu ya eneo hili iliyoko kilomita mia moja makumi sita na tano kusini-magharibi mwa Bunia./sites/default/files/2022-11/181122-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3