Habari za siku ya inne jioni
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, ujumbe mkubwa wa serikali kuu umewasili katika mji wa Goma tangu siku ya ine hii asubuhi.
- Kuhusu Ukosefu wa usalama mashariki mwa Congo, Waziri wa Ulinzi aljieleza siku ya tatu mbele ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Seneti na Bunge la Kitaifa.
- Katika Kivu Kaskazini, hali ya utulivu inatawala eneo lote linalokaliwa tangu siku sita sasa na waasi wa M23 katika eneo la usultani wa Bwisha. Iko katika tarafa la Rutshuru.
- Kushambulia wafanyakazi au mali ya MONUSCO pamoja na washirika wa serikali, katika kipindi hiki cha mzozo wa usalama huko Kivu Kaskazini, itakuwa sawa na kucheza mchezo wa adui.
- Jimboni Ituri, Mfuko wa kuwanufaisha wahasiriwa wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu umeleta tabasamu kidogo kwenye midomo ya watu wengi walioathiriwa na migogoro ya kivita mashariki mwa Kongo.
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini madaktari waliandaa maandamano katika mitaa ya Bukavu siku ya ine hii kama ishara ya huruma kwa mwenzao aliyechomwa ndani ya Hospitali ya Maboya huko Beni wiki jana.
- Katika jimbo la Maniema, mvua iliyonyesha kwa saa za mchana siku ya pili tarehe moja Novemba hadi asubuhi ya siku ya tatu tarehe tatu Novemba ikiambatana na upepo mkali ilisababisha uharibifu mkubwa wa vitu na binadamu katika manispa tatu za jiji la kindu.
- Kumewekwa mashine na vifaa kwa ajili ya mfumo wa ufuatiliaji wa ushuru wa bidhaa katika makampuni yanayotengeneza juisi za pahali, maji ya kunywa na lemonadi nyingine, bado hakuna kuelewana kati ya FEC na DGDA.
- "Uwekaji Dijitali, kipaumbele kwa maendeleo ya Afrika" ndiyo mada ya toleo la kumi na moja la Maonesho ya Africa Digital Expo ADEX 2022, yaliyofunguliwa siku ya ine hii mjini Kinshasa. makubwa katika sekta hii./sites/default/files/2022-11/03112022_-p-s-journalswahilisoir-00_web.mp3