Habari za siku ya tano asubuhi
- Zaidi ya familia elfu mbili za wahami kutoka Rutshuru na Nyiragongo, inayokuwa kwenye nafasi Don Bosco Ngangi, walipokeya siku ya tatu msaada wa chakula na vitu vingine uliotolewa na Kanisa la Methodiste Unie Kongo-Mashariki .
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, mapigano yaliripotiwa tena kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa FARDC siku ya inne hii mchana katika eneo la Kibumba.
- Katika jimbo la Ituri, shughuli za kiuchumi hazikuendeshwa leo hii siku ya inne katika vituo vingi vya ununuzi katika mtaani Irumu.
- Kufuatana na wito huu kutoka kwa jamii ya Yira ya kusimamisha shughuli za kiuchumi, msimamizi wa mtaa wa Irumu anatoa wito kwa wakaaji kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
- Jimboni Tanganyika, wakaaji wa eneo la Moliro, katika mtaa wa Moba walishutumu siku ya tatu uvamizi haramu wa sehemu ya inchi ya Kongo na jeshi la Zambia.
- Ukosefu wa usalama katika mtaa wa Kwamouth jimboni Mai-Ndombe, mwanamke aliuawa siku ya pili iliyopita huko Kwamouth na mwanajeshi wa FARDC ambaye alimpiga risasi
- Jimboni Kivu ya Kusini, gereza kuu la Uvira linapata vifaa vipya vya kusaidia kulinda usalama ya wafungwa.
- Kiongozi wa Chuo Kikuu cha Kinshasa, Profesa Jean-Marie Kayembe alizindua siku ya inne vikao via kufasiriya azarani kazi ya utafiti ku utaalam wa ikolojia ya magonjwa ya kuambukiza./sites/default/files/2022-11/181122-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3