Journal matin

Habari za siku ya inne asubuhi 

  • Tangu asubuhi mapema ya siku ya tatu , wahami waliokimbia maeneo yao ya Kanyaruchinya kufuatia habari iliyosambazwa kuhusu  kukaribia kwa waasi wamekuwa wakirejea katika maeneo hayo.
  • Jimboni Huko ya  Kivu Kaskazini, shirika UNICEF imekuwa ikiwasaidia zaidi ya wahami  elfu makumi mawili na watatu waliokimbia  kutokana na vita na M23 , kwa muda wa wiki mbili .
  • Jimboni Mai-Ndombe,  mwanabunge wa kitaifa Willy Bolio, mchaguliwa kutoka mtaa wa  Bolobo anashutumu mashambulizi ya siku hizi dhidi ya boti kwenye mto Kongo katika eneo la Kwamouth na wavamizi wenye kumiliki  silaha.
  • Bunge la Kitaifa lilianza siku ya pili  uchunguzi wa sheria unaohusiana na ushuru wa makampuni na mapato ya watu  na hata sheria  inayohusu marekebisho ya taratibu za ushuru
  • Waendesha pikipiki katika mji wa  Kolwezi jimboni  Lualaba  wamekatazwa kufanya kazi katikati mwa mji wa  Kolwezi. Uamuzi huu ulitangazwa kwao siku  ya tatu hii na  mkuu jimboni wa Lualaba.
  • Katika jimbo ya Kivu ya Kusini, safari kati ya Bukavu na Goma imekatika kabisa kwenye barabara ya kitaifa nambari mbili RN2 katika mtaawa  Kalehe.
  • Kupanda kwa bei ya bidhaa za kilimo kunaonekana katika masoko ya mji wa Matadi jimboni Kongo central. Katika soko la Minkondo, mfuko wa muhogo unatoka ku franga elfu makumi kenda hadi laki moja na makumi mbili ya franga ya kikongomani .
  • Dunia nzima ilisherehekea watu bilioni nane siku ya pili./sites/default/files/2022-11/171122-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3