Habari za siku ya inne asubuhi
- Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo haihusike na hatua yakutokununua silaha.
- Bunge la taifa lilichaguwa siku ya pili azimio la kuizuia Serikali kuanzisha mazungumzo yoyote na makundi yenyi kumiliki silaha ili kuwaingiza katika jeshi la serikali.
- Chama cha Kisiasa kimachoongozwa na bwana Moise Katumbi kilitangaza siku ya pili kuunga mkono kwa wanajeshi wa FARDC ambao wanapigana katika mashariki mwa inchi.
- Ukosefu wa usalama katika mtaa wa Bagata, hasa katika sekta ya Wamba kufuatia ukatili unaofanywa na watu wasiojulikana wenye kumiliki silaha. Msimamizi wa eneo hili ambaye ana wasiwasi, anajiuliza jinsi gani mchakato wa uchaguzi utafanyika katika eneo hili la jimbo la Kwilu.
- Katika jimbo la Kasaï-Central , kunaripotiwa mzozo mkali pa Bakua Bumba, sekta ya Mwanza-ngoma, katika mtaa wa Demba.
- Ugongwa wa Covid-19 uliongezeka kidogo kati ya mwisho wa mwezi wa kumi na mwanzoni mwa mwezi huu wa kumi na moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
- Katika Jimbo la Tshopo, zaidi ya wafanyakazi mia nne na makumi mnane wa offisi Kuu ya Mapato ya Tshopo wamepumuzishwa .
- Waendesha pikipiki na madereva wa teksi na mabasi wanakuwa tena wengi katikati ya mji wa Lubumbashi na wakisimama mahali popote hadi kufikia hatua ya kuzuia usafiri katika mji./sites/default/files/2022-11/101122-p-f-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3