Journal matin

Habari za siku ya inne asubuhi 

  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, gavana wa kijeshi anatoa wito kwa watu waliokimbia makazi yao huko Nyiragongo watulie.
  •  Kivu ya Kaskazini, kamanda mpya wa eneo la ulinzi la tatu la FARDC na Naibu Kamanda wa Kikosi cha MONUSCO walikutana ana kwa ana kwa mara ya kwanza hii siku ya tatu huko Goma.
  • Katika  Kivu ya  Kusini maandamano makubwa ya amani yalifanyika siku ya tatu hii asubuhi katika mitaa ya BUKAVU.
  •  Mahakama ya Cassation inakataa kusitisha uamuzi wa kesi inayoendelea ya Jean-Marc Kabund, aliyekuwa makamu mkuu wa ofisi ya Bunge la Kitaifa.
  •  
  • Jimboni  Ituri, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Manufaa ya Wahasiriwa wa Mahakama ya Kimataifa ya CPI yenye makao yake makuu mjini The Hague nchini Uholanzi, ambaye yuko kwenye misheni huko Bunia, anasihi kuhamasishwa kwa fedha muhimu kwa ajili ya matunzo ya maelfu ya wahasiriwa wa uhalifu uliofanywa na viongozi wa zamani wa makundi yenye silaha nchini Congo na ambao wahusika walikuwa wamehukumiwa na CPI.
  • Shirika la Fondation Bill Clinton pour la Paix linatahadharisha juu ya ongezeko la wafungwa katika magereza ya Kongo , hasa gereza kuu la Makala mjini Kinshasa.
  •  Katika jimbo la Lomami, karibu wanafunzi mia moja wa shule ya Institut Technique Médicale de Kamiji wanasomea chini ya miti baada ya mvua kubwa kuharibu majengo ya shule wiki iliyopita.
  • Zaidi ya hekta elfu makumi sita za mahindi zimepandwa katika jimbo la Haut Katanga katika muda wa miaka mitatu kutokana na ufadhili wa kilimo uliyoanzishwa na serikali ya mkoa huo./sites/default/files/2022-11/031122-p-s-jounalswahilimatin-00_web_.mp3