Matin

Habari za siku ya pili asubuhi tarehe 23/07/2024

  • Karibu watato elfu kumi wa eneo la Baswagha-Madiwe mtaani Beni katika jimbo la Kivu ya Kaskazini walipata vyeti vyao vya kuzaliwa jana siku ya kwanza mjini Beni.
  • Katika jimbo la  Kivu ya Kaskazini:  kulikuwa mzozo wakati wote wa siku ya kwanza  hii asubuhi katika eneo la Wakimbizi la Rusayo, mtaani Nyiragongo kufuatana na  mauaji ya kijana mmoja na mtu aliyevaa vazi  za kijeshi za FARDC.
  • Huko Ituri, waasi wa ADF ambao wanakimbia oparesheni za pamoja za majeshi za Kongo FARDC na Uganda UPDF katika mtaa wa  Irumu wanaendelea kusonga mbele kuelekea Mambasa.
  • Waziri mkuu Judith Suminwa anaomba wanamemba wa serikali kutumika  kwa ukweli  kwa ajili ya wanainchi ambao wanakuwa na matatizo mengi na kuatcha  matendo mabaya sawa vile wizi wa pesa ya serikali. Alisema hayo siku kwanza hii wakati wa kikao cha serikali hapa mjini Kinshasa.
  • Jimboni Kivu ya Kusini, liwali anasimamisha shughuli za uchimbaji madini kwenyi maeneo yote ya uchimbaji madini katika jimbo hilo. Jean Jacques Purusi pia anawasimamisha kazi wakuu wote wa offisi ya kukusanya mapato ya jimbo , PMR Kivu Kusini.
  • Kuhusu hatua hizi, shirika la kiraia jimboni  Kivu ya Kusini linamhimiza  liwali kuzingatia mapendekezo na matakwa yaliyotolewa na Asasi za Kiraia lakini pia na bunge la jimbo.
  • Mjini Kananga , kazi za barabara: Kampuni ya SAFRIMEX imeweka vifaa  ya kusaga udongo kwa ajili ya kuanza uwekaji wa lami katika njia mbalimbali za mji .
  • Msongamano mkubwa wa magari uanooonekana kwa kuingia mji wa Matadi:  Meya wa mji huu anakataza kuweka biashara  kando ya barabara.
  • Hakuna umeme kuanza siku ya kwanzaa hii mjini Kalemie.Kufuatana na hiyo,  Kwa sasa, REGIDESO/Kalemie haiwezi kuwapatia wakazi maji ya kunywa./sites/default/files/2024-07/230724-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3