Habari za jioni 9 Aprili, 2025
- Doha : Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya Kongo na uasi wa AFC/M23 yaliyokuwa yakitarajiwa huko Doha inchini Qatar hii siku ya tatu yameairishwa hadi tarehe ya baadaye
- Kinshasa : Waziri mkuu anatarajiwa bungeni siku ya tatu tarehe kumi na sita aprili ijayo. Wanabunge wanataka awaangaziye kuhusu mafuriko yaliyokumba mji wa Kinshasa week end iliyopita
- Bunia : Huko Ituri, asilimia makumi mbili na sita ya wanawake na watoto wachanga walikufa wakati wa kujifungua katika vituo vya afya huko Bunia mwaka jana. Kukosa kujua na uzembe wa baadhi ya wazazi ni miongoni mwa sababu za vifo hivyo vingi, waganga wazalishaji wanasema./sites/default/files/2025-04/090425-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3