Habari za jioni 08 Aprili, 2025
- KISANGANI : Jimbo la Tshopo limeathiriwa na kipindupindu. Kesi Mia mbili makumi tisa na mbili zimeripotiwa zikiwemo vifo makumi tano na saba
- KINSHASA : Baraza la Maaskofu wa Kitaifa wa Kongo (CENCO) linakaribisha uingiliaji kati wa haraka wa Serikali kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko wakati wa mvua zilizonyesha hivi karibuni katika jiji la Kinshasa
- LUBUMBASHI : Mashirika ya kiraia ya Kasumbalesa yanaomba kuimarishwa kwa usalama Katika mji huo ambako Nyumba ziliibiwa, watu walijeruhiwa kwa mapanga, mali nyingi kuchukuliwa, na mwanamke mmoja kubakwa katika usiku wa kuamkia hii siku ya pili./sites/default/files/2025-04/080425-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3