Habari za jioni 26 Februari, 2025
- Bunia : Zaidi ya familia elfu makumi tatu waliokimbia makazi yao, wahanga wa vita, wamesongamana pa Komanda kati, tangu karibu miaka minne sasa huko Ituri
- Goma : Ongezeko la vitendo vya uhalifu limeonekana mjini Goma huko Kivu Kaskazini linasema shirika la Umoja wa mataifa la Uratibu wa misaada ya kibinadamu, OCHA katika ripoti yake
- Kananga : Katika mji wa Kananga, bei ya mahindi imeshuka kwenye soko. Kipimo kinauzwa sasa franga elfu mbili mia mbili au hata elfu mbili mia tano za Kongo, badala ya elfu saba hapo mbeleni/sites/default/files/2025-02/260225-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3