Habari z'asubuhi 21 Februari, 2025
- Lubero: Milio ya risasi iliyopigwa na askari wasio fulani mchana wa hii siku ya ine pa Lubero kati ilileta hofu kwa wakazi wakizani kwamba ni ushambulizi wa M23
- Kinshasa : Liwali wa jiji la Kinshasa anaita Wakazi wa Kinshasa kuepuka kutumbukia katika ubaguzi. Daniel Bumba alisema hayo baada ya mkutano wa usalama na waziri wa mambo ya ndani
- Bunia: Huko Ituri, Hifadhi ya Wanyamapori ya Okapi, RFO, ilikamata siku ya pili Okapi huko Epulu, katika tarafa la Mambasa. Hii ni mara ya kwanza Okapi kunaswa ndani ya miaka kumi na mbili./sites/default/files/2025-02/210225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3