Habari za siku ya inne jioni tarehe 25/07/2024
- Katika jimbo la Kivu ya kaskazini, yapata watu makumi tatu na watatu waliuawa siku ya tatu na waasi wa ADF katika maeneo ya Beni na Lubero .
- Katika jimbo la Ituri, maiti ya watu wanane ziligunduliwa siku ya tatu huko UESA, karibu na kituo cha kibiashara cha Otmaber kwenye barabara ya Komanda-Luna katika usulutani wa Walesse Vonkutu kusini mwa mtaa wa Irumu
- Shirika la kiraia jimboni Ituri linaonya serikali na washirika wake kuhusu hali mbaya ya kibinadamu ya zaidi ya wakimbizi elfu makumi mbili huko Mungwalu na maeneo jirani
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini – maisha ni ngumu kabisa kwa familia za wakimbizi zinazoishi katika maeneo ya kaskazini mwa Goma
- Mji wa Kalemie umekumbwa na ongezeko la ukosefu wa usalama . Wahalifu wanao silaha huvamia nyumba ya wakaazi mara kwa mara usiku
- Matokeo ya mitihani ya serikali ya mwaka huu yameanza kutangwa tangu siku ya tatu.
- Liwali wa mji wa Kinshasa Daniel Bumba alizungumza siku ya tatu hii na Bruno Lemarquis, mwakilishi maalum makamu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo na mratibu wa masuala ya kibinadamu. Mazungumzo yao yalihusu matatizo yaokumba waazi wa Kinshasa.
- Vitabu Vitatu via sasa vinaviosemea fedha vilichapishwa rasmi siku ya inne hii hapa Kinshasa na wakaguzi wa Fedha wa IGF na kuwasilishwa katika kikao cha offisi hii ya ukaguzi wa fedha inchini Kongo
- Jamuhuri yakidemokratia ya Kongo itaandaa kongamano mwezi wa saba mwaka ujao mjini Kinshasa. /sites/default/files/2024-07/25072024-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3