Habari za siku ya tatu jioni tarehe 24/07/2024
- Kulifunguliwa siku ya tatu hii kesi dhidi ya Corneille Nangaa, kiongozi wa kundi la kisiasa na kijeshi Alliance Fleuve Congo (AFC) kwenyi Mahakama ya Kijeshi ya Kinshasa-Gombe katika gereza la Ndolo.
- Kuhusu kesi hii dhidi ya Corneille Nangaa, mwanasiasa Aisé Kanendu kutoka eneo la Lubero jimboni Kivu ya Kaskazini anaomba serikali ya Kongo kwenda mbali zaidi.
- Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa umetangaza vikwazo au adhabu dhidi ya watu watatu wanaoshutumiwa kutoa fedha kwa kundi liitwao Etat Islamique kwa kifransa katika inchi kadhaa za afrika ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako kundi hilo la kigaidi linatumika kwa jina la waasi wa ADF.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shirika la kiraia katika mtaa wa Nyiragongo linashutumu kuongezeka kwa ukosefu wa usalama unaohusisha watu wenye kumiliki silaha.
- Waziri mkuu Judith Suminwa anaomba mawaziri kufanya kazi nakuonekane matakeo mazuri. Alitoa Pendekezo hili siku ya pili wakati wakufunga kikao cha serikali .
- Katika jimbo la Ituri zaidi ya watoto elfu makumi tatu wenye umri wa kati ya miaka mitano na kumi na tano walichanjwa dhidi ya surua katika muda wa siku tano pekee katika eneo la afya la Mangala mtaani Djugu.
- Katika Jimbo la Kasai ya mashariki, kumeripotiwa ugondjwa wa kipindupindu kwa karibu miezi miwili.
- Jimboni Kivu ya kusini Regideso emekuwa ikiimarisha vifaa vyake via kazi katika mji wa Bukavu./sites/default/files/2024-07/24072024-c-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3