Journal Soir

Habari za siku ya pili jioni tarehe 23/07/2024
 

  • Bwana Jean-Bosco Bahala,  ameondolewa madaraki mwake kama kiongozi  wa Mpango wa Kupokonya Silaha PDDRC-S. Ni kulingana na amri ya rais wa jamuhuri Felix Tshisekedi iliyotangazwa siku ya pili hii mjini Kinshasa.
  • Kiongozi wa mtaa wa Fungurume, katika jimbo la Lualaba anakataza Wakaazi wa Fungurume na maeneo jirani kula samaki kutoka kando ya Mto Kelangile. Hatua hii inachukuliwa kufuatia kumwagiwa kwa bidhaa yenye sumu kwenye mto huu na gari kubwa  liliopata ajali siku ya mungu  iliyopita katika eneo hilo. 
  • Kikao cha tatu cha kongamano la kitaifa la huduma ndogo za fedha lilifunguliwa  siku ya kwanza hapa mjini Kinshasa.
  • Huko Kasai-Oriental, kuna ongezeko la bei ya mahindi katika masoko mbalimbali ya mji wa Mbuji-Mayi..
  • Liwali wa mji wa Kinshasa anaomba  wajumbe wa  baraza la usalama jimboni kutokomeza kabisa hali ya kuluna, ujambazi na msongamano wa magari mjini Kinshasa.
  • Katika jimbo la  Ituri, vikosi vya pamoja vya jeshi la FARDC na Uganda vilishambulia maeneo kadhaa ya ADF siku ya mungu katika pori ya  Mont HOYO, usulutani wa Walese Wonkutu kusini mwa mtaa wa Irumu.
  • Jimboni Kivu ya kusini, Mahakama ya kijeshi ya Uvira iliyoketi huko Mboko katika mtaa wa  Fizi iliwahukumu siku ya kwanza  askari watatu wa Fardc kwa adhabu ya kifo .
  • Liwali wa jimbo la Kongo-Central, Nkuanga Masuangi Bilolo Grace anaomba polisi na jeshi la Fardc kuimarisha juhudi zao  ya kulinda raia na mali zao kwa heshima  wa katiba.
  • Jimboni Ituri, karibu visa mia mbili vya ajali za barabarani  na vifo  makumi mbili vimehesabiwa  tangu mwanzo wa mwaka huu na polisi wa barabarani mjini Bunia.
  • Katika jimbo la Kasai-Central , chama cha kutetea haki za watoto na wanafunzi, LIZADEEL inatoa wito kwa wazazi kuchukua hatua za kulinda watoto wakati wa matokeo ya mitihani ya serikali./sites/default/files/2024-07/230724-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3