Habari za siku ya tatu jioni tarehe 10/ 07/2024
- Katika jimbo la Tshopo, wakazi wa Opienge na Balobe katika mtaa wa Bafwasende zaidi ya kilomita mia mbili na makumi sita mashariki mwa Kisangani, wanaanza kurejea hatua kwa hatua katika maeneo yao.
- Katika jimbo la Ituri, karibu familia elfu mbili za wakimbizi ambazo zimepoteza kabisa matumaini ya kurejea katika vijiji vyao vya asili katika eneo la Djugu, wameamua kuhamishwa katika maeneo yao ya makimbilio.
- Baraza la Maungamo ya Kidini la Ituri, CCRI, lanatoa wito kwa wakaaji kuongeza umakini ili kuimarisha usalama jimboni Ituri.
- Katika jimbo ya Kivu la Kaskazini, visa vya ulipizaji kisasi maarufu hurekodiwa karibu kila wiki katika mji wa Goma na mazingira yake tangu miezi kadhaa.
- Kilalo kipya kiliwekwa siku ya pili kwenye Mto Lubi huko Kena Kuna, mji mkuu wa eneo la Kabeya Kamuanga katika jimbo la Kasai Oriental.
- Kwa zaidi ya wiki moja , maji ya Regideso haitoke katika mji wa Kananga jimboni Kasai-central.
- Jimboni Koongo central , Kushuka kwa maji ya Mto Kongo inasababisha ukosefu wa maji ya kunywa katika mji wa Matadi.
- Mahakama ya Katiba imekuwa ikipokeya tangu siku ya pili tarehe kenda mwezi huu wa saba wanamemba wa serikali ambaye wanakuja kuonesha mali zao.
- Shirika linaoitwa Casmia Casmia linaohusika na ma maswala la Uchimbaji Madini, linalaani uchimbaji haramu wa madini unaofanyika Kakanda katika jimbo la Lualaba./sites/default/files/2024-07/100724-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3