Habari za siku ya tatu jioni tareha 17/01/2024
- Timu ya Leopards ya Inchi yakidemokratia ya Kongo inacheza leo hii siku ya tatu hii katika uwanja wa Laurent Mpokou mjini San Pedro nchini Cote d’Ivoire na Tshipolopolo ya Zambia.
- Kuhusu mechi hiyo , mchezaji mwakilishi wa Leopards anatoa wito kwa Wanainchi wote kuwaunga mkono kwa ushindi.
- Katika Kivu Kaskazini,jeshi la Kongo linataka kuhusika kwa shirika la Pamoja wa Uthibitishaji, kwa ajili ya kurejesha maiti ya mwanajeshi wake aliyeuawa, na kurejeshwa kwa wanajeshi wengine wawili waliokamatwa nchini Rwanda.
- Huko Ituri, Muungano wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali la kutetea haki za binadamu COARDHO inashutumu wingi wa vizuizi haramu kwenye barabara ya kitaifa nambari makumbi mbili na saba na sehemu zingine kwenye barabara ya Ezekere-Kpandroma katika mtaa wa Djugu.
- Hali ya wahami kutoka Kwamouth jimboni Maindombe Maindombe wanaoishi katika vijiji fulani katika eneo la Bagata katika jimbo la Kwilu ni mbaya sana.
- Habari njema kwa wakazi wa jimbo la Kasai Oriental kwa ujumla na hasa wale wa Mbuji Mayi.
- Habari kuhusu wizi huu wa vifaa na dawa katika hospitali kuu ya Samba katika jimbo la Maniema./sites/default/files/2024-01/17012024-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3