Habari z'asubuhi 16 Aprili, 2025
- Kinshasa : Mkutano wa kumi na sita wa Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika umefunguliwa, hii siku ya pili tarehe kumi na tano Aprili, mjini Kinshasa. Rais wa Jamhuri Felix Tshisekedi anatoa wito wa umoja wa Afrika ili kufikia malengo
- Goma : Katika Kivu Kaskazini, Waasi wa M23 waliendesha mapigano katika kijiji cha Mutao, tarafani Nyiragongo. Wakisema kwamba wanawasaka wapiganaji wa wazalendo
- Bukavu : Kanisa la Anglikana la Kongo, Dayosisi ya Bukavu, linasaidia wakimbizi wa vita na familia zinazowapokea katika mtaa wa Bagira kwa vyakula na visivyo vyakula.