Habari z'asubuhi 10 Aprili, 2025
- Kinshasa : Tangazo la Rais wa zamani Joseph Kabila kurudi inchini Kongo kupitia mji wa Goma limeleta gumzo kati ya chama tawala cha UDPS na kile cha PPRD ya Joseph Kabila. Maoni ya vyama hivyo viwili ni katika idhaa hii
- Kinshasa : Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyoikumba Kinshasa mwishoni mwa juma lililopita imeongezeka kutoka makumi tatu na tatu hadi makumi ine na tatu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku ya pili na Waziri wa Mambo ya Ndani, Jacquemain Shabani
- Kinshasa : Kampeni ya chanjo dhidi ya polio itazinduliwa hii siku ya ine tarehe kumi Aprili, inchini Kongo. Watoto wa umri wa miaka kutoka ziro hadi kumi na ine wanatarajiwa./sites/default/files/2025-04/100425-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3