Habari z'asubuhi 09 Aprili, 2025
- BENI : Mkutano wa kwanza wa moja kwa moja kati ya Serikali ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda unatarajiwa hii siku ya tatu tarehe tisa Aprili pa Doha, mji mkuu wa Qatar
- KISANGANI : Jimbo la Tshopo limeathiriwa na kipindupindu. Kesi Mia mbili makumi tisa na mbili zimeripotiwa zikiwemo vifo makumi tano na saba
- MATADI : Jimboni kongo Central, Shirika la raia la tarafa la Kasangulu, linapendekeza kusafishwa kwa Mto Lukaya, ambao una uwezekano wa kufurika hadi Kinshasa wakati wa mvua kubwa/sites/default/files/2025-04/090425-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3