Habari z'asubuhi 02 Aprili, 2025
- Genève : Mkuu wa Monusco Bi Bintou Keita aliwasilisha picha ya hali ya haki za binadamu inchini Kongo hii siku ya pili tarehe moja Aprili, wakati wa kazi ya Mazungumzo juu ya hali ya haki za binadamu nchini Kongo katika kikao cha Baraza la Haki za Kibinadamu huko Geneva
- Kisangani : Watu wa Tshopo wanaitwa kufanya biashara zao kwa amani na kutokubali habari zisizo za kweli. Wito huu ulitolewa siku ya kwanza na mkuu wa Bunge la Mkoa wa Tshopo katika ufunguzi wa kikao cha kawaida cha mwezi Machi
- Bunia : Huko Ituri, Vikosi vya Wanajeshi wa Kongo na jeshi la Uganda UPDF walizindua Siku ya kwanza mfululizo wa kampeni za kuhamasisha viongozi wa jamii kuhusu kutafuta amani ya kudumu katika tarafa la Djugu./sites/default/files/2025-04/020425-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3