Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi tarehe 30/07/2024

  • Rais wa jamhuri anatarajiwa mjini Kisangani katika jimbo la Tsopo ili kushiriki katika ukumbusho wa siku ya kwanza ya mauaji ya kitaifa ya genocost, mnamo tarehe mbili mwezi wa mnane.
  • Katika jimbo la Tanganyika, watatu wamefariki, kadhaa kujeruhiwa na zaidi ya nyumba mia moja na makumi tano kuchomwa moto. Hii ni matokeo ya muda, yanoyotelewa na shirika ya kiraia, ya uvamizi wa wanamgambo wa kundi la Bitonto asubuhi ya jana siku ya kwanza kwenye  kijiji cha Tumbwe. 
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, utulivu ilionekana siku ya kwanza  hii katika kijiji cha Ngoliba, kati ya miji ya Nyange na Bibwe, eneo la Bashali Mokoto, mtaani Masisi.
  • Katika jimbo la Kivu ya  Kaskazini tuwajulishe kwamba kuna Watoto ambao wamekuwa wasimamizi wa familia zao ambao lazima wachunge na kuwalisha kaka au dada zao wadogo.
  • Katika eneo la Beni jimboni Kivu ya Kaskazini, Kampuni ya Vihumbira (SSV), ambayo inafanya kazi ya ukarabati wa barabara ya Butembo-Manguredjipa na ujenzi wa barabara ya Manguredjipa-Bandulu, ina wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika eneo hilo.
  •  Usafiri ulikuwa ngumu siku ya kwanza hii hapa mjini Kinshasa. Madereva wa tekso waliaandaa mgomo ili  kukemea unyanyasaji unaofanywa na polisi na huduma nyingine za serikali.
  • Kuhusu matukio katika uwanja wa Martyrs wakati wa mkutano kati ya mwimbaji wa nyimbo za kumtukuza mungu  Mike Kalambay na wakazi wa Kinshasa, ambapo watu kenda walifariki na wengi kuumia siku ya sita hapa mjini Kinshasa. Kulingana na mwanamke ambaye alishiriki katika mkutano ni tabia mbaya ya ki megendo  ya wa polisi ndio msingi wa matukio haya.
  • Huko Ituri, Shirika la Biashara la Kongo FEC -ITURI, linakaribisha pendekezo la Rais wa Jamhuri Felix Tshisekedi la  kupunguza ushuru kwa waendeshaji uchumi katika jimbo la Ituri./sites/default/files/2024-07/30072024-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3