Journal matin

Habari za siku ya inne asubuhi tarehe 25/07/2024

  • Kulifunguliwa siku ya tatu hii kesi dhidi ya Corneille Nangaa, kiongozi wa kundi  la kisiasa na kijeshi Alliance Fleuve Congo (AFC) kwenyi  Mahakama ya Kijeshi ya Kinshasa-Gombe katika gereza la Ndolo. 
  • Kuhusu kesi hii dhidi ya Corneille Nangaa, mwanasiasa Aisé Kanendu kutoka eneo la Lubero jimboni Kivu ya Kaskazini anaomba serikali ya Kongo kwenda mbali zaidi. 
  • Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa umetangaza vikwazo au adhabu  dhidi ya watu watatu wanaoshutumiwa kutoa fedha kwa kundi liitwao Etat Islamique kwa kifransa katika inchi kadhaa za afrika ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako kundi hilo la kigaidi linatumika kwa jina la waasi wa ADF.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shirika la kiraia katika mtaa wa Nyiragongo linashutumu kuongezeka kwa ukosefu wa usalama unaohusisha watu wenye kumiliki  silaha. 
  • Waziri mkuu Judith Suminwa anaomba mawaziri kufanya kazi nakuonekane  matakeo mazuri. Alitoa Pendekezo hili siku ya pili wakati wakufunga kikao cha serikali .
  • Katika jimbo la  Ituri zaidi ya watoto elfu makumi tatu  wenye umri wa kati ya miaka mitano na kumi na tano walichanjwa dhidi ya surua katika muda wa siku tano pekee katika eneo la afya la Mangala mtaani Djugu.
  • Katika Jimbo la Kasai ya  mashariki, kumeripotiwa ugondjwa  wa kipindupindu kwa karibu miezi miwili.  
  • Jimboni Kivu ya kusini Regideso emekuwa ikiimarisha vifaa vyake via kazi katika mji wa Bukavu./sites/default/files/2024-07/25072024-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3