Journal matin

Habari za siku ya inne asubuhi  tarehe 18/07/2024

  • Ni lazima kwa  haraka  kuchukua hatua zinazofaa ili kuimarisha usalama na udhibiti katika mpaka nambari kumi na tatu kati ya inchi la Kongo na Rwanda". Haya ni madai ya Waziri Mkuu makamu wa jamuhuri ya kidemokratia ya Kongo aneyehusika na Mambo ya Ndani na usalama, alipomaliza kazi yake katika  jimbo la Kivu ya kaskazini
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, mzozo ilikuwa juu asubuhi yote ya siku ya tatu hii katika wilaya ya Majengo, kaskazini mwa Goma na katika kijiji cha Turunga, kusini mwa eneo jirani la Nyiragongo.
  • Katika jimbo la Kivu  ya Kaskazini, watu wawili waliuawa katika mashambulizi matatu tofauti siku ya kwanza na siku ya pili  zidi ya misafara ya jeshi la Uganda na jeshi la Kongo, pamoja na nafasi ya jeshi la  FARDC katika eneo la kutoka kusini mwa mji wa Butembo.
  • Huko Ituri, angalau asilimia makumi saba  ya watu ambao walikuwa wamekimbia unyanyasaji wa makundi yenye silaha katika eneo la Irumu kuelekea eneo la Komanda-Luna tayari wamerejea katika vijiji vyao .
  • Mjini Kinshasa, mauaji, ubakaji na unyang'anyi wa kutumia silaha ni aina mpya ya uhalifu unaokumba wakaaji wa mitaa inne za wilaya ya Funa. Hizi ni Bumbu, Ngiri-ngiri, Selembao na Makala. 
  • Kuongezeka kwa uhalifu huko Kalemie:  meya wa mji anatangaza kwamba polisi wamechukua hatua fulani ili kupiganisha  jambo hili.
  • Usafiri kwenyi  barabara kati ya mji wa Bukavu na mji mkuu wa eneo la Mwenga yanakuwa magumu kutokana na uchakavu wa kilalo la Ulindi kwenye mto Ulindi. 
  • Katika jimbo la Lomami, kwa kupita kwa magari makubwa juu ya kilalo cha la Luilu katika katika mtaa wa Luilu  sasa kunmelizumishwa usafirishaji wa bidhaa.
  • Katika jimbo la Mai-Ndombe kwamba  viongozi  wa shule ya Saint Benoît iliyoko katika kijiji cha Masiambio katika eneo la Kwamouth, wanaomba serikali na watu wenye mioyo mema, msaada wa majengo, vifaa na vifaa vya shule kwa ajili ya shule hii./sites/default/files/2024-07/180724-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3