Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi tarehe 12/12/2023

  • Kufanyika kwa uchaguzi tarehe makumi mbili mwezi huu wa kumi na mbili  na jambo la ukosefu wa usalama na hali mbaya ya kibinadamu nchini Kongo yakidemokratia ndio kabisa msingi  wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu inchi la Kongo.
  • Akizungumza mbele ya Baraza la Usalama kwa niaba ya mashirika ya kiraia nchini DRC, Sandrine Lusamba, Mratibu wa Kitaifa wa Mshikamano wa Wanawake kwa Amani, aliangazia hasa matokeo ya ukosefu wa usalama nchini humo.
  • Katika jimbo la Kivu Kaskazini,  mji wa Goma pamoja na mji wa  Sake, karibu kuatchanishwa kabisa mbali na barabara tatu muhimu za huduma za kilimo ambazo zinawaunganisha na eneo lote la Masisi.
  • Kuondolewa kwa wanajeshi wa kikosi cha EAC-RF inchini Kongo , karibu wa askari  mia kenda wa kikosi cha Burundi waliondoka Goma wikendi hii. Ni baada yakuondoka kwa vikosi via  Kenya na Sudan ya Kusini.
  • Katika jimbo la Kivu ya  Kusini, zaidi ya visa elfu makumi inne na tatu vya surua vilihesabiwa kutoka  mwezi wa kwanza hadi  mwezi wa kumi na mbili mwaka huu  katika maeneo makumi tatu inne ya afya.
  • Dola za kimarekani bilioni mia tatu ndio fedhza ya kibajeti itakayokusanywa kwa kipindi cha miaka kumi ili kutekeleza mpango wa serikali ya Adolphe MUZITO endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri.
  • Kuhusu Biashara ya mafuta kwenye mpaka wa Kavimvira, katika mji wa Uvira, jimboni Kivu Kusini./sites/default/files/2023-12/121223-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3