Daktari Babah Mutuza : Wakati wa jua kali tuepuke maji isiwaishe watoto mwilini

Katika jiji la Beni, wataalamu wa afya wanatoa wito kwa wakazi kuwa makini sana na masuala ya afya katika kipindi hiki cha jua kali ambacho kimeshuhudiwa katika eneo hilo tangu katikati ya mwezi wa Desemba. Kwa mujibu wao, kipindi hiki kina madhara ya moja kwa moja kwa afya ya binadamu kama vile upungufu wa maji mwilini, kikohozi, homa na mengine. Watu walioathirika zaidi ni wazee na watoto. Ni hatua gani za kuzuia afya zinapaswa kuzingatiwa katika hali hii? Tunazungumza juu yake na mkurugenzi wa matibabu wa kliniki ya Dieu est Grand katika jiji la Beni jimboni Kivu Kaskazini; Daktari Babah Mutuza akizungumza na Marc Maro Fimbo.

/sites/default/files/2025-01/280125-p-s-invitebenidrbabahmutuzasecheresse-00-web.mp3