Mwezi Desemba iliyopita, Umoja wa Ulaya ulipiga marufuku uidhinishaji wa makampuni yanayosafirisha kahawa na kakao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hii ni hasa kwa lengo la kukatisha tamaa ukataji miti na wizi katika sekta ya ununuzi wa bidhaa hizo unaoibua tamaa ya makundi yenye silaha. Waendeshaji wengi wa kiuchumi na wakulima wanaona hatua hii kuwa haifai, hasa katika maeneo ya Beni huko Kivu Kaskazini na Mambasa huko Ituri na Tshopo ambako wakazi wengi wanaishi kutokana na bidhaa hizi. Mgeni wetu Serge Kambale mtaalam wa sekta ya kahawa na kakao anazungumzia madhara ya uamuzi huu katika mahojiano haya na Ezechiel MUZALIA.
/sites/default/files/2025-01/240125-p-s-invitebuniasergekambaleexpertcacao-00-web.mp3