Tunamkaribisha kama mgeni afisa mawasiliano wa mbuga la wanyama la Virunga. Bienvenu Bwende anatueleza kuhusu athari za eneo la viwanda lililoundwa miaka miwili iliyopita na Alliance Virunga huko Munigi, katika tarafa la Nyiragongo. Eneo hili, ambalo ni la pili baada ya lile la Mutwanga katika tarafa la Beni, lina malengo mawili: kusaidia kulinda rasilimali za mbuga la wanyama la Virunga na kuunda uchumi mbadala kwa jamii jirani. Je, malengo haya yamefikiwa miaka miwili baadaye? Majibu ya Bienvenu Bwende katika mahojiano haya na Bernardin Nyangi.
/sites/default/files/2024-05/230524-p-s-invitegomabienvenubwendeiccn-00-web.mp3