Habari za siku ya pili jioni tarehe 30/07/2024
- Watu makumi mbili walifariki na wengine wengi kupotea : haya ni matokeo ya muda ya kuzama kwa mashua ndogo siku ya mungu jioni huko KAMBOLÉ mjini Kindu katika jimbo la Maniema.
- Katika jimbo la Kivu ya kusini, Moto uliwaka siku ya pili hii katika kituo cha mafuta huko Bukavu karibu na hospitali kuu ya Bukavu. Matokeo ya muda ni watu watatu kujeruhiwa vibaya, nyumba mbili, magari mawili na pikipiki mbili zilizochomwa moto.
- Jimboni Kivu ya kaskazini, mradi wa STAR-EST, ambao ni mradi wa Uimarishaji na ukarabati wa barabara Mashariki mwa Kongo ulizinduliwa siku kwa kwanza Mjini Beni .
- Hapa mjini Kinshasa, ujumbe wa Benki ya Dunia, ukiongozwa na Mkurugenzi wake anayehusika na operesheni , Bwana Albert Zeufack, uliwasilisha siku ya kwanza kwa Waziri wa Elimu , Raissa Malu, mfuko yakukuza elimi unayokadiriwa kwa dolla za marekani milliari mmoja na nukta inne.
- Huko Ituri, soko la UZI lililoko kilomita makumi kenda na tatu kaskazini mwa Bunia katika eneo la PIMBO mtaani Djugu linafanya limeanza tena kutumikishwa baada ya miaka sita ya kufungwa kwake kufuatia unyanyasaji ya makundi yenye kumiliki silaha.
- Jamuhuri ya Kidemokratia ya Kongo inashutumu Rwanda kwa kuvuruga mawasiliano yake ya anga ambayo kulingana na viongozi wa Kongo inahatarisha usalama wa usafiri wa anga nchini.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, utulivu ulionekana siku ya pili hii huko Katwe, katika eneo la Mutanda , usulutani wa Bwito mtaani Rutshuru baada ya mapigano kati ya waasi wa m23 na wapiganaji kutoka kundi la CMC/FAPC la Jonas Bigabo usiku wa wakuamkiya siku ya pili hii.
- Hali imekuwa ya wasiwasi kwa siku tatu katika eneo la magharibi la la Bashali Mokoto, mtaani Masisi.
- Wafanyakzi wa Kampuni ya Usafiri ya Kongo (Transco) wanaamua kusitisha mgomo wao siku ya pili hii , baada ya kulipwa kwa mishahara yao ya miezi miwili na Waziri wa Fedha.
- Usafiri hapa Kinshasa umerejea kama kawaida katika sehemu kubwa ya mji ./sites/default/files/2024-07/30072024-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3