Habari za siku ya tano jioni tarehe 16/06/2023
- Katika jimbo la Ituri, watu kumi na watano waliuawa na nyumba kumi na mbili kuchomwa wakati wa shambulio jipya la waasi wa ADF jana siku ya inne katika eneo la Bandavilemba kusini mwa mtaa wa Irumu.
- Jimboni Kivu ya Kusini, vijana wa mji wa Bukavu wamejianda kabisa kwa ushiriki mkubwa katika mchakato wa uchaguzi.
- Kwa kutarajia Siku kuuu ulimwenguni ya Mtoto wa Afrika inayosherekewa leo hii tarehe kumi na sita mwezi wa sita, watoto wapasha habari wa Unicef walifanya kampeni siku ya inne iliyopita ya uhamasishaji juu ya ulinzi wa mazingira.
- Jimbo la Kongo Central ni miongoni mwa majimbo yanayoshiriki katika kikoa cha kumi na nane cha wiki ya madini ya Kongo ya Kidemokratia ambayo inafanyika mjini Lubumbashi.
- Jimboni Tanganyika, mkuu wa eneo la Kauwa katika usulutani wa Bena Mambwe, mtaani la Kongolo aliachiliwa jana na wanamungambo Maimai. Kulingana na msimamizi makamu wa mtaa wa Kongolo, wa maimai hawa kutoka emtaa wa Kabambare huko Maniema walishambulia eneo hili siku ya kwanza iliyopita .
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, hali ya usalama bado ni ya wasiwasi leo hii katika maeneo kadhaa ya mtaa wa Masisi.Ni jana ndio kikao cha kawaida cha mwezi wa tatu kilikomeshwa katika bunge la taifa ./sites/default/files/2023-06/160623-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3